UMBA DUNIA YAKO, ISHI DUNIA YAKO NA SHINDANA NA WEWE. 09:52 daileth mbele 1 "Maisha ni safari, uwe na mwelekeo wako binafsi." Nyumbani ni mahala ambapo moyo wako upo. Mahala ambapo moyo wako upo ni sehemu ambayo kuna watu unaowapenda kwa dhati, moyo wako ulipo ni pale ambapo una uhakika kuna watu wanaokupenda. Moyo wako ulipo ni sehemu ambayo kuna mazingira unayoyapenda na kuna vitu unavyovipenda. Kuishi dunia yako ni kuishi kwa kuongozwa na ndoto zako, ni kuishi kwa kufanya yanayokupa furaha ya kweli. Kuishi dunia yako ni kutaka na kufanya vitu kadiri ya vipaji vyako, uzoefu wako, na uwezo wako. Maisha ni safari na sisi sote tu wasafiri. Safari hii kila mtu ana usafiri anaotumia ili kufika ukomo wa safari yake. Kadhalika kila mtu anapaswa kufahamu wapi hasa ana kwenda au wapi hasa anataka kufika na kwa nini anataka kufika huko anako kwenda, yaani madhumuni ya safari yake ni nini, ni muhimu kufahamu pia muda kiasi gani utatumika kufikia anayoyataka. Maisha yanaongozwa na malengo, hayaongozwi na hisia, tamaa, au kuiga iga wenzako. Watu wengi wanaojitambua hapa duniani wana ndoto au mipango wanayoipigania kuitimiza. Yapo mambo ambayo kila wakilala wanawaza jinsi watakavyoyafanikishi, alfajiri ikifika wanasali wakiamini kuwa huenda ikawa ndiyo siku ya kutimiza ndoto zao. Wengine hata wakitembea barabarani wanawaza na kuwazua watatimiza vipi maono yao. Fahamu kuwa kila mtu duniani hapa ni pekee na upekee wake uanzia kwenye jinsi anavyofikiri, ndoto za mafanikio anazoziota, wakati anaotaka ziwe zimetimia na tunatofautiana pia katika njia tunazoaamini zinaweza kutuletea mafanikio. Tunaweza kuota ndoto moja lakini tukatofautiana kuhusu vipi na lini itatimia. Hali ya mtu kupenda anachokipenda na kutaka anachokitaka, ndiyo tunaita kujitambua. Mtu anaposhindwa kutambua anahitaji nini, wakati gani, kwa nini na kwa jinsi gani tunasema hajitambui. Yaani anaishi bila sababu. Ni kifuata upepo. Vifuata upepo katika dunia ya leo ni wengi sana. Tapia hii ipo kwa watu wazima, vijana na mpaka watoto. Watoto wanaathiriwa zaidi na mienendo ya wazazi. Watu wengi wanafanya mambo wasiyoyapenda ili waridhishe watu au ili wapate sifa za watu. Mathalani nilienda kumtembelea mtu mmoja ninanayefahamiana nae kwa muda mrefu. Nilipofika kwake nikakuta amenunua gari zuri sana la kutembelea. Wakati nikimpongeza kwa furaha zote, akanambia kitu kilichonifanya nimshangae sana. Aliniambia " Ndugu niliamua kununua gari hili baada ya kuona watu karibia wote ofisini kwangu wamenunua magari, na wengine wana mipango ya kununua nikaona nikope mkope bank ili nami niendeshe". Nilimtazama kwa macho ya kumuhurumia, nikabaini kutojitambua kwake japo amenizidi umri. Siku zimepita sasa nagundua kuisha kwa kujilinganisha na kujishindanisha, kufanya hili na lile kwa sababu ya kutafuta sifa au kuogopa kuonekana wadhaifu ni tabia mbaya, na kasumba mbaya ambayo inazaa ugonjwa sasa. Watu wengi hawaishi uhalisia wao, wananunua magari kwa sababu wengine wamenunua, wanasoma kwa sababu wengine wanasoma na hata wanajenga kwa sababu wengine wanajenga. Kushindana na watu hakuna manufaa, ni hasara kwa sababu kila mtu anaishi ndoto zake, kadhalika hakuna mtu anaweza kuwajuu ya watu wote katika jamii yake. Mathalani unaweza kuwa na gari lakini ukakosa nyumba, ukawa na nyumba ukakosa familia, ukawa na mamilioni lakini ukakosa furaha, ajabu wasio na fedha za kutosha ndiyo utawaona wakifurahi. Kushindana kimaisha bila mipaka na bila hekima ni kujiumiza tu akili, roho na mwili. Ni kujinyima furaha ya maisha kwa makusudi. Mfano, unapokuwa unafanya vitu kwa kushindana na mtu fulani maana yake unaacha malengo yako uliyojipangia, unaanza kutimiza malengo ya mtu mwingine. Mfano mtu amejipanga kununua gari, wewe unapomuana anaendesha anaendesha ndoto zake za muda mrefu. Wewe ukimuona ukamuiga basi ujue unatimiza ndoto za mwenzako. Unapotimiza ndoto za mwenzio kuna mawili kuhusu ndoto zako. Moja, ndoto zako zitasahaulika na kubaki kwenye ubongo au kwenye karatasi. Pili,Utakosa furaha ya maisha kwa sababu vitu vingi unavyovifanya si matokeo ya mawazo yako na maono yako, matokeo yake muda mwingi utajikuta una mrundikano wa vitu vingi kichwani ambavyo havijatekelezwa kama matokeo ya kukosa msimamo wa mipango uliyojiwekea. Watu wengi wameweka rehani furaha zao kama matokeo ya kuishi kimapambano na watu wengine. Wengi fulani afanya nini ndiyo kunaamua yeye afanye nini. Fulani amevaa nini ndo kunaamua yeye avae nini, fulani anasoma nini ndiyo sababu ya yeye kusoma. Fahamu kuwa kushindana bila hekima ni tabia ya watu dhaifu, watu imara wanaishi ndoto zao. Watu imara hawaishi mawazo ya watu wengine bila kujiongeza. Kushindana ni utoto na ni kupoteza muda, panga mipango yako na pigania kuitekeleza. Ukiona unaishi kwa kuangalia wenzako wamefanya nini na wewe ndo ufanye, ukiona hauna mipango unayoipigania, ukiona haushughulishi kutaka kujua unachotaka maishani mwako basi fahamu tayari uko mateka. Mateka wa maisha ya mashindano, yaani uko miongoni mwa watu wanoishi bila malengo. Vifuata upepo. Kama wewe ni mwanafunzi shindana na A’s, B’s, C’s na shindana malengo yako kitaaluma uliyojiwekea kwamba. Mfano shindana kuwa mtu unaye muota kuwa, mfano shindana kuwa daktari, mwalimu, mwanasheria, mwandishi, mhasibu n.k. Usishindane na watu. USISHINDANE NA WATU BALI SHINDANA NA MIPANGO YAKO. ISHI NDOTO ZAKO. Daileth I. Mbele, Simu 0746492600 Blogu: chemchemi3.blogspot.com/ Jifahamu UMBA DUNIA YAKO, ISHI DUNIA YAKO NA SHINDANA NA WEWE. " Maisha ni safari, uwe na mwelekeo wako binafsi ." Nyumbani ni mahala ambapo moyo wako upo. Mahala ambapo moyo wako upo ni se... Read more »