Haitatokea katika kategoria hii ya mkasa tukachapisha kisa cha uongo wala cha kubuni.Visa na mikasa yote itakayochapishwa katika blogu hii ni vile vya kweli na vyenye uthibitisho wa ukweli huo. Maana lengo la kipengele hiki ni kujifunza, kufurahi na kuyatafakari maisha zaidi ya tunavyoyatafakari.
Leo naomba nianze na kisa hiki ambacho kimetokea mji kasoro bahari, Morogoro. Lakini kwa sababu ya kulinda utu na kuzingatia maadili ya habari majina ya wahusika wa kisa hiki sitayataja. Ila ni kisa kibichi kabisa ambacho bado ni habari ya mtaa mmoja wapo ambapo kimetokea. Nami nimekishuhudia.
Ndugu mmoja mwanaume alianza mahusiano na binti ambaye bado alikuwa anaishi kwao yaani kwa wazazi wake. Baada ya mahusiano yao kuzidi kukua na penzi lao kustawi wakaona watambulishane kwa wazazia kama mwanzo wa mchakato wa kufunga ndoa.
Siku zikaenda mapenzi yakazidi kuwa moto moto kweli huku ndugu jamaa wakitarajia wakati wowote ndoa itafungwa. Sasa penzi lao likawa si la kificho tena, yaani kila kitu hadharani. Mwanaume akawa wakati analala kwa binti, binti asipoonekana nyumbani familia haikusumbuka, kumtafuta walijua pakumpata!
Penzi likazidi kunoga hatimaye mwanaume akahamia kwa mwanamke, yaani ukweni. Maisha yakaendelea, siku zikasonga.. familia ikampokea kijana wa kiume kama mtoto wao .
Mara bundi akalia ndani ya penzi lao, migogoro mara kwa mara ,jitihada za usuluhishi hazikuzaa matunda hatimaye binti akaona hawezikuendelea na huyo kijana. Akachukua vitu vyake na kumwacha mwanaume akiendelea kuishi kwa wakwe zake wakati binti aliyemleta ameondoka zake!
Bila aibu mwanaume aliendelea kuishi na wazazi wa binti aliyeachanae kwa zaidi ya mwezi mmoja mpaka familia ya binti ilipomkalia kikao cha kumtaka aondoke maana undugu haupo tena, penzi lililowaunganisha limekwisha vunjika.
Nachojiuliza mimi huyu jamaa alitaka aendelee kuishi hapo mpaka lini na kwa malengo gani. Alitegemea watarudiana siku moja au alitegemea nini hasa hata kukaa kwa wazazi wa binti uliyeachana naye bila hofu!Dunia ina mambo, ukishangaa ya Musa Utayaona ya Firauni .
Nawe binti unayesoma hapa, usipeleke mwanaume nyumbani alafu mnagombana unamuacha, hakikisha umemtoa kwanza. Usiwaachie watu kero.
Mwaume usipende mterermko kupindukia,unakimbiliaje kirahisi tu kwenda kuishi kwao na mwanamke!
CHEMCHEMI3.BLOGSPOT.COM#DARASA LA MAISHA
Post a Comment