Banner Chemchemi3 Blog; Darasa lako Maisha,Kliniki yako ya maisha | Darasa La Maisha - Maisha Mafanikio

0


"Miasha ni zawadi . Ifurahie. Maisha ni safari, uwe na mwelekeo(malengo)"
Maisha yana maana unapojitambua wewe ni nani na ukaishi kadiri ya uhalisia wako. Kujitambua ni kupana mno. Mtu anaanza kujitambua akiwa tumboni mwa mama na anapozaliwa anaendelea kujitambua.

Kujitambua hakuna ukomo, hakuna kuhitimu ndiyo kusema maisha ni kujifunza kila siku ya Mungu. Binadamu anajifunza mpaka siku anayorejea kwa muumba wake. Ukomo wa kujitambua ni kifo. Anayekoma kutaka kujitambua angali hai huyo ni mfu anayeishi.


Blog hii ni sehemu ya wewe kufahamu kwa nini unaishi. Unaishi kwa sababu zipi na dunia inanufaika vipi na uwepo wako hapa ulimwenguni. Hii ni blog ya kukufanya uishi kwa malengo, na kuacha kuishi kwa mazoea. Ukiwa msomaji wa blog hii kila siku utaiona siku ya thamani na hautaitumia kwa hasara na hatimaye maisha yako yatakuwa ya mafanikio.

Tiba mbadala ya tabia hasi. Kuna watu wengi wamekwama katika tabia zenye matokeo mabaya kwenye maisha yao. Wamejizoesha tabia zenye kuathiri ustawi wao wa kiroho, kiakili na hata kimwili. Blog hii ni sehemu sahihi kwako uliye katika changamoto za kimwenendo. Hii ni hospitali yako.

Yako maradhi ambayo hayatibiki hospitalini lakini yanadhurumu maisha ya watu na familia nyingi. Kadiri utakavyotembelea blog hii utatibika pia utajigundua kama wewe ni muhanga.

Furaha ni haki na zawadi yako. Maisha yafaa nini kama huna furaha moyoni mwako. Furaha huumbwa, huambukizwa. Blog hii kama ilivyo jina lake ni chemchemi ya furaha. Msomaji wa blog hii hapa ndipo penye chemchemi nzuri ya raha na amani.

Wakati watu wengi wanatumia starehe hatarishi ili wapate furaha matokeo yake bado wanajikuta wanapungukiwa. Mimi nakushauri kuwa msomaji wa blog hii na utakuwa na furaha tele. Tena furaha halisi ya kutoka ndani.

Kuna watu wanatazama maisha kwa macho ya kijuu juu blog hii itakufanya ufahamu zaidi ya unavyofahamu. Maisha yako hayatakuwa kama jana baada ya kuwa msomaji wa blog hii. Kama muendeshaji wa blog niseme tu nakupenda sana.

KARIBU CHEMCHEMI3.BLOGSPOT.COM NI DARASA LA MAISHA. KLINIKI YA MAISHA YAKO




Next
Newer Post
Previous
This is the last post.

Post a Comment

 
Top